7. Hata itakuwa, wote wakutazamao watakukimbia, wakisema, Ninawi umeharibika; ni nani atakayeuhurumia? Nikutafutie wapi wafariji?
8. Je! Wewe u mwema kuliko No-amoni, uliowekwa kati ya mito, uliozungukwa na maji; ambao boma lake lilikuwa bahari, na bahari ilikuwa ukuta wake.
9. Kushi na Misri walikuwa nguvu zake, nazo zilikuwa hazina mpaka; Putu na Walibia walikuwa wasaidizi wake.
10. Hata hivyo alichukuliwa mbali, alikwenda utumwani; watoto wake wachanga walisetwa kwenye maachano ya njia kuu zote; watu wake wenye heshima wakapigiwa kura, na wakuu wake wote wakafungwa kwa minyororo.
11. Tena utalewa, utafichwa; tena utatafuta ngome kwa sababu ya adui.
12. Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva kwanza; ikitikisika zaanguka katika kinywa chake alaye.
13. Tazama, watu wako walio ndani yako ni wanawake; malango ya nchi yako yamekuwa wazi kabisa mbele ya adui zako; moto umeteketeza mapingo yako.
14. Teka maji yawe tayari kwa kuzingirwa kwako;Zitie nguvu ngome zako;Ingia katika udongo, yakanyage matope,Itie nguvu tanuru ya kuokea matofali.
15. Huko moto utakuteketeza;Upanga utakukatilia mbali;Utakumeza kama tunutu alavyo;Jifanye kuwa wengi kama tunutu!Jifanye kuwa wengi kama nzige!