1. Yeye asetaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana.
2. Kwa maana BWANA anairudisha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli; maana watekao nyara wamewateka, na kuyaharibu matawi ya mizabibu yao.
3. Ngao ya mashujaa wake imefanywa kuwa nyekundu, watu walio hodari wa vita wamevaa nguo nyekundu sana; magari ya vita yametameta kwa chuma cha pua siku ya kujitengeza kwake, na mikuki inatikiswa kwa namna ya kutisha.
4. Magari ya vita yanafanya mshindo njiani,Yanasongana-songana katika njia kuu;Kuonekana kwake ni kama mienge,Yanakwenda upesi kama umeme.
5. Awakumbuka watu wake wenye heshima;Wanajikwaa katika mwendo wao;Wanafanya haraka waende ukutani;Nacho kitu cha kuwafunika kimewekwa tayari.