Mwa. 6:9-13 Swahili Union Version (SUV)

9. Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.

10. Nuhu akazaa wana watatu wa kiume, Shemu, na Hamu, na Yafethi.

11. Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma.

12. Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani.

13. Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.

Mwa. 6