Mwa. 49:2-7 Swahili Union Version (SUV)

2. Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo,Msikilizeni Israeli, baba yenu.

3. Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza,Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu.Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.

4. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu,Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako,Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.

5. Simeoni na Lawi ni ndugu;Panga zao ni silaha za jeuri.

6. Nafsi yangu, usiingie katika siri yao,Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao,Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu,Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng’ombe;

7. Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali,Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma.Nitawagawa katika Yakobo,Nitawatawanya katika Israeli.

Mwa. 49