13. Zabuloni atakaa pwani ya bahari,Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu,Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
14. Isakari ni punda hodari,Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo;
15. Akaona mahali pa raha, kuwa pema,Na nchi, ya kuwa ni nzuri,Akainama bega lake lichukue mizigo,Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.
16. Dani atahukumu watu wake,Kama moja ya makabila ya Israeli;
17. Dani atakuwa nyoka barabarani,Bafe katika njia,Aumaye visigino vya farasi,Hata apandaye ataanguka chali.
18. Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.