Mwa. 33:7-10 Swahili Union Version (SUV)

7. Lea naye, na wanawe, wakakaribia wakainama. Baadaye Yusufu na Raheli wakakaribia, wakainama.

8. Akasema, Kundi hili lote nililolikuta, maana yake ni nini? Akasema, Kunipatia kibali machoni pa bwana wangu.

9. Esau akasema, Ninayo tele, ndugu yangu, uliyo nayo na yawe yako.

10. Yakobo akasema, Sivyo; kama nimekubalika machoni pako tafadhali upokee zawadi yangu mkononi mwangu, iwapo nimeona uso wako kama kuona uso wa Mungu, ukapendezwa nami.

Mwa. 33