Mwa. 30:10-19 Swahili Union Version (SUV)

10. Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana.

11. Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi.

12. Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana wa pili.

13. Lea akasema, Ni heri mimi, maana wanawake wataniita heri. Akamwita jina lake Asheri.

14. Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao.

15. Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo kuninyang’anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao.

16. Yakobo akaja kutoka kondeni jioni, Lea akatoka kumlaki, akasema, Lazima uje kwangu, kwa sababu nimekuajiri, kwa tunguja za mwanangu; akalala kwake usiku ule.

17. Mungu akamsikia Lea, naye akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana wa tano.

18. Lea akasema, Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nimempa mume wangu mjakazi wangu. Akamwita jina lake Isakari.

19. Lea akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa sita.

Mwa. 30