Mwa. 11:6-18 Swahili Union Version (SUV)

6. BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.

7. Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.

8. Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.

9. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.

10. Hivi ndivyo vizazi vya Shemu; Shemu alikuwa mtu wa miaka mia akamzaa Arfaksadi miaka miwili baada ya gharika.

11. Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, waume na wake.

12. Arfaksadi akaishi miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela.

13. Arfaksadi akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na wake.

14. Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi.

15. Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, waume na wake.

16. Eberi akaishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi.

17. Eberi akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, waume na wake.

18. Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa Reu.

Mwa. 11