21. Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
22. Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,
23. Tazama, bikira atachukua mimba,Naye atazaa mwana;Nao watamwita jina lake Imanueli;Yaani, Mungu pamoja nasi.
24. Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;
25. asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.