Mk. 9:45-50 Swahili Union Version (SUV)

45. Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [

46. ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]

47. Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;

48. ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.

49. Kwa sababu kila mtu atatiwa chumvi kwa moto.

50. Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.

Mk. 9