1. Mara kulipokuwa asubuhi wakuu wa makuhani walifanya shauri pamoja na wazee na waandishi na baraza nzima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta mbele ya Pilato.
2. Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu, akamwambia, Wewe wasema.
3. Nao wakuu wa makuhani walikuwa wakimshitaki mambo mengi.
4. Pilato akamwuliza tena akisema, Hujibu neno? Tazama ni mambo mangapi wanayokushitaki!
5. Wala Yesu hakujibu neno tena, hata Pilato akastaajabu.
6. Basi wakati wa sikukuu huwafungulia mfungwa mmoja, wamwombaye.