Mk. 14:17-20 Swahili Union Version (SUV)

17. Basi ilipokuwa jioni yuaja pamoja na wale Thenashara.

18. Nao walipokuwa wameketi chakulani, wakila, Yesu alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu, naye anakula pamoja nami, atanisaliti.

19. Wakaanza kuhuzunika, wakamwambia mmoja mmoja, Je! Ni mimi?

20. Akawaambia, Ni mmoja wa hao Thenashara, ambaye achovya pamoja nami katika kombe.

Mk. 14