1. Akaondoka huko akafika mipakani mwa Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.
2. Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu.
3. Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini?
4. Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.
5. Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.
6. Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
7. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;