Mit. 8:29-35 Swahili Union Version (SUV)

29. Alipoipa bahari mpaka wake,Kwamba maji yake yasiasi amri yake;Alipoiagiza misingi ya nchi;

30. Ndipo nilipokuwa pamoja naye, kama stadi wa kazi;Nikawa furaha yake kila siku;Nikifurahi daima mbele zake;

31. Nikiifurahia dunia inayokaliwa na watu;Na furaha yangu ilikuwa pamoja na wanadamu.

32. Basi, wanangu, nisikilizeni sasa;Maana heri hao wazishikao amri zangu.

33. Sikieni mafundisho, mpate hekima,Wala msiikatae.

34. Ana heri mtu yule anisikilizaye,Akisubiri sikuzote malangoni pangu,Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.

35. Maana yeye anionaye mimi aona uzima,Naye atapata kibali kwa BWANA.

Mit. 8