22. Uendapo yatakuongoza, ulalapo yatakulinda,Na uamkapo yatazungumza nawe.
23. Maana maagizo hayo ni taa, na sheria hiyo ni nuru,Na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima.
24. Yakulinde na mwanamke mwovu, asikupate,Na kukuponya na ubembelezi wa mgeni.
25. Usiutamani uzuri wake moyoni mwako;Wala usikubali akunase kwa kope za macho yake.
26. Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate;Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani
27. Je! Mtu aweza kuua moto kifuani pake,Na nguo zake zisiteketezwe?
28. Je! Mtu aweza kukanyaga makaa ya moto,Na nyayo zake zisiungue?
29. Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake;Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.
30. Watu hawamdharau mwivi,Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa;