Mit. 31:9-16 Swahili Union Version (SUV)

9. Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki;Uwapatie maskini na wahitaji haki yao.

10. Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?Maana kima chake chapita kima cha marijani.

11. Moyo wa mumewe humwamini,Wala hatakosa kupata mapato.

12. Humtendea mema wala si mabaya,Siku zote za maisha yake.

13. Hutafuta sufu na kitani;Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.

14. Afanana na merikebu za biashara;Huleta chakula chake kutoka mbali.

15. Tena huamka, kabla haujaisha usiku;Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;Na wajakazi wake sehemu zao.

16. Huangalia shamba, akalinunua;Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.

Mit. 31