21. Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake;Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22. Hujifanyia mazulia ya urembo;Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23. Mume wake hujulikana malangoni;Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24. Hufanya nguo za kitani na kuziuza;Huwapa wafanya biashara mishipi.
25. Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;Anaucheka wakati ujao.
26. Hufumbua kinywa chake kwa hekima,Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
27. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake;Wala hali chakula cha uvivu.
28. Wanawe huondoka na kumwita heri;Mumewe naye humsifu, na kusema,
29. Binti za watu wengi wamefanya mema,Lakini wewe umewapita wote.
30. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
31. Mpe mapato ya mikono yake,Na matendo yake yamsifu malangoni.