Mit. 31:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.

2. Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu?Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?

3. Usiwape wanawake nguvu zako;Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.

4. Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme;Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?

5. Wasije wakanywa na kuisahau sheria,Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.

6. Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea;Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.

7. Anywe akausahau umaskini wake;Asiikumbuke tena taabu yake.

8. Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu;Uwatetee watu wote walioachwa peke yao;

Mit. 31