1. Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.
2. Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu?Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?
3. Usiwape wanawake nguvu zako;Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.
4. Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme;Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?
5. Wasije wakanywa na kuisahau sheria,Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.
6. Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea;Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.