29. Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza,Naam, wanne walio na mwendo mzuri.
30. Simba aliye hodari kupita wanyama wote;Wala hajiepushi na aliye yote;
31. Jimbi aendaye tambo; na beberu;Na mfalme ambaye haasiki.
32. Ikiwa umefanya kipumbavu kwa kujikuza;Au ikiwa umewaza mabaya;Basi weka mkono wako juu ya kinywa chako.
33. Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi;Na kupiga pua hutokeza damu;kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.