21. Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini,Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
22. Msikilize baba yako aliyekuzaa,Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
23. Inunue kweli, wala usiiuze;Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu.
24. Baba yake mwenye haki atashangilia;Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia.
25. Na wafurahi baba yako na mama yako;Na afurahi aliyekuzaa.
26. Mwanangu, nipe moyo wako;Macho yako yapendezwe na njia zangu.
27. Kwa maana kahaba ni shimo refu;Na malaya ni rima jembamba.
28. Naam, huotea kama mnyang’anyi;Huwaongeza wenye hila katika wanadamu.
29. Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?Ni nani aliye na macho mekundu?
30. Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo;Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31. Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32. Mwisho wake huuma kama nyoka;Huchoma kama fira.
33. Macho yako yataona mambo mageni;Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari;Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.