Mit. 21:2-12 Swahili Union Version (SUV)

2. Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe;Bali BWANA huipima mioyo.

3. Kutenda haki na hukumuHumpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.

4. Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari,Hata ukulima wa waovu, ni dhambi.

5. Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu;Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.

6. Kupata akiba ya mali kwa ulimi wa uongoNi moshi upeperushwao; ni kutafuta mauti.

7. Jeuri ya wabaya itawaondolea mbali;Kwa sababu wamekataa kutenda hukumu.

8. Njia yake aliyelemewa na dhambi imepotoka sana;Bali mtu aliye safi, kazi yake ni sawasawa.

9. Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini,Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.

10. Nafsi ya mtu mbaya hutamani uovu;Jirani yake hapati fadhili machoni pake.

11. Mwenye mzaha aadhibiwapo, mjinga hupata hekima;Na mwenye hekima afundishwapo, hupokea maarifa.

12. Mwenye haki huitafakari nyumba ya mtu mbaya;Jinsi wabaya waangushwavyo wakaangamia.

Mit. 21