Mhu. 8:8-12 Swahili Union Version (SUV)

8. Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho;Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa;Wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile;Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.

9. Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.

10. Pia nikaona waovu wamezikwa, nao wamefika kaburini; tena waliofanya mema wameondoka katika patakatifu, nao wamesahauliwa mjini. Hayo nayo ni ubatili.

11. Kwa sababu hukumu juu ya tendo baya haitekelezwi upesi, mioyo ya wanadamu huthibitishwa ndani yao ili kutenda mabaya.

12. Ajapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia, akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake;

Mhu. 8