18. Kwa sababu ya uvivu paa hunepa;Na kwa utepetevu wa mikono nyumba huvuja.
19. Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko,Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.
20. Usimlaani mfalme, la, hata katika wazo lako;Wala usiwalaani wakwasi chumbani mwako;Kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti,Na mwenye mabawa ataitoa habari.