1. Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume.
2. Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu.
3. Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.
4. Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno.