15. Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;
16. akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
17. Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?
18. Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?
19. Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.
20. Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;
21. wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.