Lk. 10:26-31 Swahili Union Version (SUV)

26. Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

27. Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

28. Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.

29. Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?

30. Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.

31. Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.

Lk. 10