Law. 21:10-20 Swahili Union Version (SUV)

10. Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake;

11. wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake;

12. wala asitoke katika mahali patakatifu, wala asipatie unajisi mahali patakatifu pa Mungu wake; kwa kuwa utakaso wa hayo mafuta ya kutiwa ya Mungu wake u juu yake; mimi ndimi BWANA.

13. Naye atamwoa mwanamke katika ubikira wake.

14. Asitwae mjane, wala mwanamke aliyeachwa na mumewe, wala mwanamke mwenye unajisi, wala kahaba; lakini atamwoa mwanamwali katika watu wake mwenyewe.

15. Naye asiwatie unajisi kizazi chake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi BWANA nimtakasaye.

16. Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

17. Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

18. Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili,

19. au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,

20. au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;

Law. 21