Kut. 5:6-10 Swahili Union Version (SUV)

6. Na siku ile ile Farao akawaamuru wasimamizi wa watu, na wanyapara wao, akisema,

7. Msiwape watu tena majani ya kufanyia matofali, kama mlivyofanya tangu hapo; na waende wakatafute majani wenyewe.

8. Lakini hesabu ya matofali waliyokuwa wakifanya tokea hapo, wawekeeni iyo hiyo, msiipunguze hata kidogo, kwa maana ni wavivu hao; kwa hiyo wanapiga kelele, wakisema, Tupe ruhusa twende kumtolea Mungu wetu dhabihu.

9. Wapeni watu hao kazi nzito zaidi, waitaabikie; wala wasiangalie maneno ya uongo.

10. Hao wasimamizi wa watu na wanyapara wao wakatoka, wakasema na watu, wakanena, Farao asema hivi, Mimi siwapi majani.

Kut. 5