Kut. 40:30-38 Swahili Union Version (SUV)

30. Akaliweka birika kati ya hema ya kukutania na madhabahu, akatia maji ndani yake ya kuoshea.

31. Musa na Haruni, na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yake;

32. hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu walinawa kama BWANA alivyomwamuru Musa.

33. Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.

34. Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.

35. Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.

36. Na hapo lile wingu lilipoinuliwa kutoka juu ya maskani, wana wa Israeli wakaenda mbele katika safari zao zote,

37. bali kama lile wingu halikuinuliwa, wakati ule hawakusafiri hata siku ile lilipoinuliwa tena.

38. Kwa maana lile wingu la BWANA lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.

Kut. 40