Kut. 40:11-14 Swahili Union Version (SUV)

11. Kisha utalitia mafuta birika na tako lake, na kuliweka liwe takatifu.

12. Kisha utamleta Haruni na wanawe hapo mlangoni pa hema ya kukutania, nawe utawaosha kwa maji.

13. Kisha utamvika Haruni mavazi matakatifu; nawe utamtia mafuta, na kumweka awe mtakatifu, ili apate kunitumikia katika kazi ya ukuhani.

14. Kisha utawaleta wanawe, na kuwavika kanzu zao;

Kut. 40