42. Sawasawa na yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyoifanya hiyo kazi yote wana wa Israeli.
43. Musa akaiona hiyo kazi yote, na tazama, walikuwa wameimaliza; vile vile kama BWANA alivyoagiza, walikuwa wameifanya vivyo; basi Musa akawaombea heri.