Kut. 36:24-34 Swahili Union Version (SUV)

24. naye akafanya matako ya fedha arobaini yawe chini ya hizo mbao ishirini; matako mawili chini ya ubao mmoja kwa hizo ndimi zake mbili, na matako mawili chini ya ubao mwingine kwa ndimi zake mbili.

25. Na kwa upande wa pili wa maskani upande wa kaskazini, akafanya mbao ishirini,

26. na matako yake ya fedha arobaini; matako mawili chini ya ubao mmoja, na matako mawili chini ya ubao mwingine.

27. Na kwa upande wa nyuma wa hiyo maskani kuelekea magharibi akafanya mbao sita.

28. Naye akafanya mbao mbili kwa pembe za maskani upande wa nyuma.

29. Nazo zilikuwa mbao pacha upande wa chini, vivyo zilishikamana pamoja hata ncha ya juu kufikilia pete ya kwanza; ndivyo alivyofanya zote mbili katika hizo pembe mbili.

30. Hivyo zilikuwa mbao nane, na matako yake ya fedha, matako kumi na sita, matako mawili chini ya kila ubao.

31. Kisha akafanya mataruma ya miti ya mshita; matano kwa mbao za upande mmoja wa maskani;

32. na mataruma matano kwa mbao za upande wa pili wa maskani, na mataruma matano kwa hizo mbao za maskani zilizokuwa upande wa nyuma kuelekea magharibi.

33. Naye akalifanya hilo taruma la katikati lipenye kati ya hizo mbao kutoka upande huu hata upande huu.

34. Naye akazifunika hizo mbao dhahabu, akazifanya zile pete zake za dhahabu ziwe mahali pa hayo mataruma, akayafunika dhahabu hayo mataruma.

Kut. 36