33. Kwamba mtu atafunua shimo, au kuchimba shimo, naye asilifunike, kisha ikawa ng’ombe au punda kutumbukia humo,
34. mwenye shimo atalipa; atampa huyo mwenye mnyama fedha, na mnyama aliyekufa atakuwa ni wake.
35. Ng’ombe wa mtu akimwumiza ng’ombe wa mtu mwingine hata akafa; ndipo watamwuza huyo ng’ombe aliye hai na kugawanya thamani yake; na ng’ombe aliyekufa pia watamgawanya.
36. Au kwamba ilijulikana ya kuwa ng’ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng’ombe kwa ng’ombe, na huyo ng’ombe aliyekufa atakuwa ni wake.