Kut. 2:23-25 Swahili Union Version (SUV)

23. Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.

24. Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo.

25. Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia.

Kut. 2