Kut. 15:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema,Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana;Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.

2. BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu;Naye amekuwa wokovu wangu.Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu;Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.

3. BWANA ni mtu wa vita,BWANA ndilo jina lake.

4. Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini,Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.

5. Vilindi vimewafunikiza,Walizama vilindini kama jiwe.

6. BWANA, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo,BWANA, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui.

7. Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea,Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu.

8. Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa,Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu,Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.

9. Adui akasema, Nitafuatia, nitapata, nitagawanya nyara,Nafsi yangu itashibishwa na wao;Nitaufuta upanga wangu, mkono wangu utawaangamiza.

Kut. 15