Kum. 6:11-23 Swahili Union Version (SUV)

11. na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vimefukuliwa usivyofukua wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba;

12. ndipo ujitunze, usije ukamsahau BWANA aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa.

13. Mche BWANA, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.

14. Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;

15. kwani BWANA, Mungu wako, aliye katikati yako ni Mungu mwenye wivu; isije ikawaka juu yako hasira ya BWANA, Mungu wako, akakuangamiza kutoka juu ya uso wa nchi.

16. Msimjaribu BWANA, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu huko Masa.

17. Zishikeni kwa bidii sheria za BWANA, Mungu wenu, na mashuhudizo yake, na amri zake alizokuagiza.

18. Nawe fanya yaliyo sawa, na mema, machoni pa BWANA; ili mpate kufanikiwa, nawe upate kuingia na kuimiliki nchi nzuri BWANA aliyowaapia baba zako,

19. ya kuwa atawasukumia nje adui zako wote mbele yako, kama alivyosema BWANA.

20. Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, N’nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu?

21. Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu;

22. BWANA akaonya ishara na maajabu, makubwa, mazito, juu ya Misri, na juu ya Farao, na juu ya nyumba yake yote, mbele ya macho yetu;

23. akatutoa huko ili kututia huku, apate kutupa nchi aliyowaapia baba zetu.

Kum. 6