20. Na Gadi akamnena,Na abarikiwe amwongezaye Gadi;Yeye hukaa kama simba mke,Hurarua mkono, naam, na utosi wa kichwa.
21. Akajichagulia sehemu ya kwanza,Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria;Akaja pamoja na wakuu wa watu,Akaitekeleza haki ya BWANA,Na hukumu zake kwa Israeli.
22. Na Dani akamnena,Dani ni mwana-simba,Arukaye kutoka Bashani.
23. Na Naftali akamnena,Ee Naftali, uliyeshiba fadhili,Uliyejawa na baraka ya BWANA;Umiliki magharibi na kusini.
24. Na Asheri akamnena,Na abarikiwe Asheri kwa watoto;Na akubaliwe katika nduguze,Na achovye mguu wake katika mafuta.
25. Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba;Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.
26. Hapana aliyefanana na Mungu, Ee Yeshuruni,Ajaye amepanda juu ya mbingu ili akusaidie.Na juu ya mawingu katika utukufu wake.
27. Mungu wa milele ndiye makazi yako,Na mikono ya milele i chini yako.Na mbele yako amemsukumia mbali adui;Akasema, Angamiza.