Kum. 32:43-50 Swahili Union Version (SUV)

43. Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake;Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake,Atawatoza kisasi adui zake,Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake.

44. Musa akaja akasema maneno haya yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua, mwana wa Nuni.

45. Musa akamaliza kuwaambia Israeli wote maneno haya yote;

46. akawaambia, Yawekeni mioyoni mwenu maneno yote ambayo nashuhudia kwenu hivi leo; nayo waamuruni watoto wenu, wayatunze na kuyafanya maneno yote ya torati hii.

47. Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.

48. BWANA akasema na Musa siku iyo hiyo, akamwambia,

49. Kwea katika mlima huu wa Abarimu, mpaka kilima cha Nebo, kilicho katika nchi ya Moabu, kuelekea Yeriko; ukaangalie nchi ya Kanaani niwapayo wana wa Israeli kuimiliki;

50. ukafe katika kilima, huko ukweako, ukusanywe uwe pamoja na jamaa zako; kama alivyokufa nduguyo Haruni katika mlima wa Hori, akakusanywa awe pamoja na watu wake;

Kum. 32