Kum. 32:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena;Na nchi isikie maneno ya kinywa changu.

2. Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua,Maneno yangu yatatona-tona kama umande;Kama manyunyu juu ya majani mabichi;Kama matone ya mvua juu ya mimea.

3. Maana nitalitangaza Jina la BWANA;Mpeni ukuu Mungu wetu.

4. Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu;Maana, njia zake zote ni haki.Mungu wa uaminifu, asiye na uovu,Yeye ndiye mwenye haki na adili.

5. Wametenda mambo ya uharibifu,Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao;Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka.

6. Je! Mnamlipa BWANA hivi,Enyi watu wapumbavu na ujinga?Je! Yeye siye baba yako aliyekununua?Amekufanya, na kukuweka imara.

7. Kumbuka siku za kale,Tafakari miaka ya vizazi vingi;Mwulize baba yako, naye atakuonyesha;Wazee wako, nao watakuambia.

8. Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao,Alipowabagua wanadamu,Aliweka mipaka ya watuKwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.

Kum. 32