Kum. 28:40-46 Swahili Union Version (SUV)

40. Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika.

41. Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu watakwenda utumwani.

42. Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa nayo.

43. Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.

44. Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia.

45. Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza;

46. nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele;

Kum. 28