5. Kisha BWANA akasema nami mara ya pili, akaniambia,
6. Kwa sababu watu hawa wameyakataa maji ya Shiloa yapitayo polepole, na kufurahi kwa ajili ya Resini na huyo mwana wa Remalia,
7. basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo Mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote, atafurika juu ya kingo zake zote;
8. naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.
9. Fanyeni ghasia, enyi kabila za watu,Nanyi mtavunjwa vipande vipande;Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali;Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande;Jikazeni viuno, nanyi mtavunjwa vipande vipande.
10. Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika;Semeni neno, lakini halitasimama;Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
11. Maana BWANA aliniambia hivi, kwa mkono hodari, akanifundisha nisiende katika njia ya watu hawa, akisema,
12. Msiseme, Ni fitina, katika habari za mambo yote ambayo watu hawa watasema, Ni fitina; msihofu kwa hofu yao, wala msiogope.
13. BWANA wa majeshi ndiye mtakayemtakasa; na awe yeye hofu yenu, na awe yeye utisho wenu.
14. Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.
15. Na wengi watajikwaa juu yake, na kuanguka na kuvunjika, na kunaswa na kukamatwa.
16. Ufunge huo ushuhuda, ukaitie muhuri sheria kati ya wanafunzi wangu.
17. Nami nitamngojea BWANA, awafichaye uso wake nyumba ya Yakobo, nami nitamtazamia.