1. Ni nani huyu atokaye Edomu,Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra?Huyu aliye na nguo za fahari,Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake?Mimi nisemaye kwa haki,Hodari wa kuokoa.
2. Kwani mavazi yako kuwa mekundu,Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu?
3. Nalikanyaga shinikizoni peke yangu;Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami;Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu,Naliwaponda kwa ghadhabu yangu;Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao,Nami nimezichafua nguo zangu zote.
4. Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu,Na mwaka wao niliowakomboa umewadia.