Isa. 60:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja,Na utukufu wa BWANA umekuzukia.

2. Maana, tazama, giza litaifunika dunia,Na giza kuu litazifunika kabila za watu;Bali BWANA atakuzukia wewe,Na utukufu wake utaonekana juu yako.

3. Na mataifa wataijilia nuru yako,Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka kwako.

4. Inua macho yako, utazame pande zote;Wote wanakusanyana; wanakujia wewe;Wana wako watakuja kutoka mbali.Na binti zako watabebwa nyongani.

5. Ndipo utakapoona na kutiwa nuru,Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka;Kwa kuwa wingi wa bahari utageuzwa kukujia,Utajiri wa mataifa utakuwasilia.

6. Wingi wa ngamia utakufunika,Ngamia vijana wa Midiani na Efa;Wote watakuja kutoka Sheba;Wataleta dhahabu na uvumba;Na kuzitangaza sifa za BWANA.

7. Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako,Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia;Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali,Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu.

8. Ni nani hawa warukao kama wingu,Na kama njiwa waendao madirishani kwao?

Isa. 60