6. Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,Mwiteni, maadamu yu karibu;
7. Mtu mbaya na aache njia yake,Na mtu asiye haki aache mawazo yake;Na amrudie BWANA,Naye atamrehemu;Na arejee kwa Mungu wetu,Naye atamsamehe kabisa.
8. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
9. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
10. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
11. ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
12. Maana mtatoka kwa furaha,Mtaongozwa kwa amani;Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo;Na miti yote ya kondeni itapiga makofi.
13. Badala ya michongoma utamea msunobari,Na badala ya mibigili, mhadesi;Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina,Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.