Isa. 53:7-12 Swahili Union Version (SUV)

7. Alionewa, lakini alinyenyekea,Wala hakufunua kinywa chake;Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni,Na kama vile kondoo anyamazavyoMbele yao wakatao manyoya yake;Naam, hakufunua kinywa chake.

8. Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa;Na maisha yake ni nani atakayeisimulia?Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai;Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.

9. Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya;Na pamoja na matajiri katika kufa kwake;Ingawa hakutenda jeuri,Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.

10. Lakini BWANA aliridhika kumchubua;Amemhuzunisha;Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi,Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi,Na mapenzi ya BWANA yatafanikiwa mkononi mwake;

11. Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika.Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye hakiAtawafanya wengi kuwa wenye haki;Naye atayachukua maovu yao.

12. Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu,Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari;Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa,Akahesabiwa pamoja na hao wakosao.Walakini alichukua dhambi za watu wengi,Na kuwaombea wakosaji.

Isa. 53