4. Hakika ameyachukua masikitiko yetu,Amejitwika huzuni zetu;Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa,Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
5. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,Alichubuliwa kwa maovu yetu;Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake,Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
6. Sisi sote kama kondoo tumepotea;Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe;Na BWANA ameweka juu yakeMaovu yetu sisi sote.
7. Alionewa, lakini alinyenyekea,Wala hakufunua kinywa chake;Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni,Na kama vile kondoo anyamazavyoMbele yao wakatao manyoya yake;Naam, hakufunua kinywa chake.
8. Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa;Na maisha yake ni nani atakayeisimulia?Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai;Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
9. Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya;Na pamoja na matajiri katika kufa kwake;Ingawa hakutenda jeuri,Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.