1. Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni;Jivike mavazi yako mazuri,Ee Yerusalemu, mji mtakatifu;Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yakoAsiyetahiriwa, wala aliye najisi.
2. Jikung’ute mavumbi; uondoke,Uketi, Ee Yerusalemu;Jifungulie vifungo vya shingo yako,Ee binti Sayuni uliyefungwa.
3. Maana BWANA asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha.