21. watu wale niliojiumbia nafsi yangu, ili wazitangaze sifa zangu.
22. Lakini hukuniita, Ee Yakobo, bali umechoka nami, Ee Israeli.
23. Hukuniletea wana-kondoo kuwa kafara zako, wala hukuniheshimu kwa dhabihu zako. Sikukutumikisha kwa matoleo, wala sikukuchosha kwa ubani.
24. Hukuninunulia manukato kwa fedha, wala hukunishibisha kwa mafuta ya sadaka zako; bali umenitumikisha kwa dhambi zako, umenichosha kwa maovu yako.
25. Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
26. Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.
27. Baba yako wa kwanza alifanya dhambi, na wakalimani wako wameniasi.
28. Kwa hiyo nitawatia unajisi wakuu wa patakatifu, nami nitamfanya Yakobo kuwalaani, na Israeli kuwa tukano.