29. Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
30. Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;
31. bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.